Posts

Kambi maalum ya matibabu na upimaji wa moyo yafanyika Zanzibar

Image
Afisa Uuguzi wa Taasisi  ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) John Mirisho akimpima kipimo cha kuangalia wingi wa sukari mwilini Othman Maulid aliyefika katika Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja Zanzibar leo kwa ajili ya kupata huduma ya  upimaji na matibabu ya moyo. JKCI kwa kushirikiana na Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar wanafanyaka kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku tano kwa watoto na watu wazima. Mtafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Makrina Komba akimuuliza maswali mama Mwajuma Kidawa aliyefika leo katika Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja Zanzibar kwa ajili ya kupata huduma ya upimaji na matibabu ya moyo yanayofanyika katika hospitali hiyo. JKCI kwa kushirikiana na Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar wanafanyaka kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku tano kwa watoto na watu wazima. Afisa Uuguzi wa Taasisi   ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)    Tumpale Kionjola akimpima shinikizo la damu mwilini (BP) mama Amina Marzuk aliyefika katika Hospita...

Tanzania na China zasaini muhtasari wa taarifa ya upembuzi yakinifu ya u...

Image

Matibabu ya moyo yaanza kutolewa JKCI Dar Group

Image

Tanzania na China zasaini muhtasari wa taarifa ya upembuzi yakinifu ya ujenzi na upanuzi wa JKCI

Image
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu na Kansela wa Uchumi na Biashara kutoka Ubalozi wa China Nchini Tanzania Chu Kun wakisaini muhtasari wa taarifa ya upembuzi yakinifu ya ujenzi na upanuzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) katika eneo la Mloganzila lililopo wilayani Ubungo jijini Dar es Salaam. Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu pamoja na Kansela wa Uchumi na Biashara kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania Chu Kun wakionesha muhtasari wa taarifa ya upembuzi yakinifu ya ujenzi na upanuzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) katika eneo la Mloganzila mara baada ya kusaini muhtasari huo leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.  Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu akielezea namna ambavyo Serikali kupitia Wizara ya Afya imejipanga kuboresha miundombinu ya afya wakati wa kusaini muhtasari wa taarifa ya upembuzi yakinifu ya ujenzi na upanuzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) katika eneo la Mloganzila lililopo wilayani Ubungo...

Waziri Ummy: Igeni JKCI kutokupokea rushwa

Image
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) baada ya kufanya ziara yake katika Hospitali ya JKCI Dar Group leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia huduma zinazotolwa na Hospitali hiyo. Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na wagonjwa wanaotibiwa katika Hospitali ya JKCI Dar Group alipotembelea Hospitali hiyo leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia huduma zinazotolewa.  Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akikagua maeneo ya Hospitali ya JKCI Dar Group alipotembelea Hospitali hiyo leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia huduma zinazotolewa. Kaimu Mkurugenzi Hospitali ya JKCI Dar Group Dkt. Tulizo Shem akimwelezea Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu huduma zinazotolewa katika Hospitali hiyo alipotembelea JKCI Dar Group kwa ajili ya kuangalia huduma zake leo jijini Dar es Salaam Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu alipote...

Ubalozi wa China watembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete

Image
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angella Muhozya akimuonesha moja ya chumba cha kulipia (VIP) Kansela wa Uchumi na Biashara kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania Chu Kun alipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuangalia huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa. Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo na mfumo wa umeme wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Yona Gandye akielezea huduma zinazotolewa katika chumba cha upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua (Cathlab) wakati Kansela wa Uchumi na Biashara kutoka Ubalozi wa china nchini Tanzania Chu Kun alipotembelea JKCI leo kwa ajili ya kuangalia huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angella Muhozya akimuelezea huduma zinazotolewa na Taasisi hiyo Kansela wa Uchumi na Biashara kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania Chu Kun alipotembelea JKCI leo kwa ajili ya kuangalia huduma za matibabu ya moyo zinazot...

Dkt. Kisenge: Fanyeni kazi kwa kufuata maadili ya utumishi wa umma

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wafanyakazi wapya 57 walioajiriwa na Serikali kupitia Sekretariate ya Ajira na kupangiwa kutoa huduma katika Taasisi hiyo wakati akifungua mafunzo yaliyofanyika  leo katika ukumbi wa JKCI jijini Dar es Salaam. Baadhi ya Wafanyakazi wapya 57 walioajiriwa na Serikali kupitia Sekretariate ya Ajira na kupangiwa kituo cha kazi  katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa wakati wa mafunzo elekezi kwa  wafanyakazi hao yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam. Daktari bingwa wa upasuaji Alex Msoka akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wafanyakazi wapya 57 walioajiriwa na Serikali kupitia Sekretariate ya Ajira ambao wamepangiwa kituo cha kazi katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa mafunzo elekezi kwa  wafanyakazi yaliyofanyika  leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. ...