JKCI yafungua kliniki inayotumia mashine za Akili Unde (AI) SABASABA

 

Fundi sanifu wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mussa Omary akimpima mfumo wa umeme wa moyo mkazi wa Dar es Salaam aliyetembelea kliniki ya JKCI iliyopo katika maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiangalia mashine inayotumia akili unde (AI) kufanya usajiri kwa kumulika sura ya mgonjwa wakati wa uzinduzi wa kliniki ya taasisi hiyo iliyopo katika maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge, viongozi wa Taasisi hiyo na washiriki wa maonesho ya SABASABA wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzinduzi kliniki ya JKCI iliyopo katika maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.


Afisa Tehema wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Kliniki ya Osterbay Suleiman Jaffer akimuelezea Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Peter Kisenge namna kifaa maalumu cha DOZEE kinavyofanya kazi wakati wa uzinduzi wa kliniki ya taasisi hiyo iliyopo katika maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiangalia mashine inayotumia akili unde (AI) kufanya usajiri kwa kumulika sura ya mgonjwa wakati wa uzinduzi wa kliniki ya taasisi hiyo iliyopo katika maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Pcha na JKCI

*********************************************************************************************************************************************************************
Na Mwandishi-Maalumu.
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) yafungua Kliniki inayotumia mashine za Akili Unde (AI) kutoa huduma za usajili na matibabu kwa wananchi wanaotembelea banda la Taasisi hiyo lililopo katika maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biasharaya Dar es Salaam (SABASABA). 

Mashine hizo zina uwezo wa kumsajiri mwananchi anayetaka kupata hudumu kwa kuweka sura yake na kutambua taarifa zake zote muhimu hivyo kupunguza msongamano wa usajiri na muda wa kupata huduma.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kliniki hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alisema Taasisi hiyo imeanzisha Kliniki katika maonesho hayo ili kuwapa wananchi nafasi ya kupata huduma za ushauri, uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo.

 “JKCI ni fahari ya Tanzania kutokana na uwezo wake wa kutumia teknolojia za kisasa zinazorahisisha utoaji wa huduma za afya kimataifa ambapo mgonjwa hupata huduma kwa muda mfupi kuanzia anapofika katika usajili hadi kufanyiwa uchunguzi na matibabu” alisema Dkt. Kisenge.

Dkt. Kisenge ambaye pia ni dakatari bingwa wa magonjwa ya moyo aliwataka wananchi wajitokeze kwa wingi kutembelea katika banda la Taasisi hiyo ili waweze kupata huduma na kujionea vifaa vyenye teknologia ya kisasa vinavyotumika katika matibabu mbalimbali ya moyo ikiwemo upasuaji wa moyo.

“Miongoni mwa teknologia zinazooneshwa katika banda letu ni pamoja na kifaa kinachotumia shuka maalumu la “Dozee” ambacho hufuatilia hali ya mgonjwa akiwa nyumbani kwa kupima mapigo ya moyo na viashiria vingine muhimu vya afya bila kumlazimu mgonjwa kufika hospitalini”, alisema Dkt. Kisenge. 

Kwa upande wake Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Thabiti Kombo Ramadhani alisema wananchi wanaotembelea banda la JKCI wanapata fursa ya kupimwa vipimo vya awali vinavyoweza kusababisha magonjwa ya moyo bila gharama ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuzuia magonjwa yasiyoambukiza kupitia kampeni ya Jua Namba Zako.

Dkt. Kombo alisema sambamba na kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wananchi wanaotembelea banda la hilo pia JKCI iwemeka huduma za maonesho kuionesha jamii JKCI inavyofanya kazi kwa kutumia teknolojia za kisasa.

Dkt. Kombo aliongeza kuwa huduma zote za msingi zinazotolewa na Taasisi hiyo sasa zinapatikana katika kliniki iliyopo katika maonesho ya SABASABA ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kusogeza huduma za kibingwa na ubingwa bobezi karibu na wananchi.


Comments

Popular posts from this blog

Kutoka miaka 22 hadi kustaafu: Safari ya Lemmah yatoa somo kwa Watumishi wa Umma

Wanawake waaswa kulinda mioyo yao, kuepuka sukari na chumvi kupita kiasi