SERIKALI YASAINI MAKUBALIANO YA MAFUNZO YA HUDUMA ZA UBINGWA BOBEZI KUTOKA MISRI.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya ALAMEDA kutoka MISRI wamesaini makubaliano yatayotoa fursa kwa Wataalamu wa afya kutoka Tanzania kupata mafunzo ya huduma bobezi zakibingwa kutoka kwa Wataalamu wa Hospitali hiyo ya Misri, jambo litalonufaisha Watanzania kwa huduma hizo. Prof. Makubi ameyasema hayo, leo Oktoba 20, 2022 katika tukio la kusaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano pamoja na Mtendaji Mkuu wa Alameda Healthcare Group kutoka nchi ya Misri Bw. Neeraj Mishra ikiwa ni sehemu ya kuboresha ushirikiano wa kimataifa baina ya nchi hizo, tukio lililofanyika katika ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma. “Leo Oktoba 20, 2022 tumesaini makubaliano ya pamoja yatayosaidia kuboresha huduma ikiwemo kunufaika kwa watalaamu zaidi ya 20 kila mwaka kutokana na mafunzo kwa watumishi wa afya katika nyanja za ubingwa na ubingwa bobezi watayoendelea kupata kutoka kwa Wataalamu wa nchi ya Misri.” Amesema Prof. Makubi. Ameendelea kusema ...