Chama cha madaktari bingwa wa kupandikizaji vifaa na tiba ya mfumo wa umeme wa moyo kuboresha huduma kwa wagonjwa
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo Johnson Lwakatare
akimkabidhi muongozi wa chama Rais wa Chama cha Madaktari Bingwa wa
upandikizaji vifaa na tiba ya magonjwa ya mfumo wa umeme wa moyo (Device and
arrhythmia society of Tanzania) Dkt. Yona Gandye wakati wa uzinduzi wa chama
hicho uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Rais wa Chama cha Madaktari Bingwa wa upandikizaji vifaa na tiba ya magonjwa ya mfumo wa umeme wa moyo (Device and arrhythmia society of Tanzania) Dkt. Yona Gandye akizungumza na wanachama wa chama hicho jana wakati wa uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Chama cha Madaktari Bingwa wa upandikizaji vifaa na tiba ya magonjwa ya mfumo wa umeme wa moyo (Device and arrhythmia society of Tanzania) Dkt. Khuzeima Khanbhai akielezea malengo ya chama hicho jana wakati wa uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Rais wa Chama cha Madaktari bingwa wa magonjwa ya ndani
Tanzania Mwanaada Kilima akiwapongeza wataalamu wanaotoa huduma za matibabu ya
mfumo wa umeme wa moyo wakati wa uzinduzi wa Chama cha Madaktari Bingwa wa
upandikizaji vifaa na tiba ya magonjwa ya mfumo wa umeme wa moyo (Device and
arrhythmia society of Tanzania) uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wataalamu wa afya wakifuatilia yaliyokuwa
yakiendelea wakati wa uzinduzi wa Chama cha Madaktari Bingwa wa upandikizaji
vifaa na tiba ya magonjwa ya mfumo wa umeme wa moyo (Device and arrhythmia
society of Tanzania) uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Picha na: Khamis Mussa
********************************************************************************************************
Na Khamisi Mussa - Dar es Salaam
Madaktari wa moyo wanaotoa huduma za matibabu kwa wagonjwa
wenye matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo waandika historia kwa kuanzisha Chama cha
madaktari bingwa wa upandikizaji vifaa na tiba ya magonjwa ya mfumo wa umeme wa
moyo (Device and arrhythmia society of Tanzania).
Akizungumza jana wakati wa uzinduzi wa chama hicho Rais wa
Chama Dkt. Yona Gandye alisema madaktari wanaotoa huduma kwa wagonjwa wenye
matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo wameungana kwa pamoja na kukutanisha wadau
mbalimbali duniani kujadili namna ya kutatua changamoto ambazo wagonjwa hao
wamekuwa wakipia.
Dkt. Gandye ambaye pia ni Daktari bingwa wa moyo Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) alisema katika mkutano huo wamejadiliana na kuona
changamoto katika kutoa huduma kwani wanatambua hiyo ni moja ya huduma ambayo
hapa nchini haijapewa kipaumbele kutokana na uchache wa wataalamu na maeneo ya
kutoa huduma kuwa machache.
“Tumeweza kutengeneza mikakati na kuongeza ufahamu kwa
wataalamu wa afya wengine ili kutoa fursa kwa wagonjwa wenye matatizo hayo
kupata huduma sehemu tofauti na kutibiwa kwa wakati”, alisema Dkt. Gandye
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Dkt. Peter
Kisenge alisema matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo ni makubwa na yanachangia
vifo vingi duniani huku wengine wakipoteza maisha wakiwa na umri mdogo.
Dkt. Kisenge alisema sababu zinazosababisha matatizo ya mfumo
wa umeme wa moyo ni pamoja na magonjwa ya mishipa ya damu ama magonjwa ya
kuzaliwa nayo yanayoweza kupelekea hitilafu katika mfumo wa umeme wa moyo.
“Uwepo wa chama hiki utasaidia kutoa mafunzo kwa wataalamu wa afya katika hatua mbalimbali za kitaaluma lakini kutoa mafunzo ya namna wagonjwa hao wanatakiwa kufanya pale anapogundulika kuwa na tatizo la mfumo wa umeme wa moyo”, alisema Dkt. Kisenge
Naye Rais wa Chama cha Madaktari bingwa wa magonjwa ya ndani
Tanzania Mwanaada Kilima alisema Tanzania inajivunia kuanzishwa kwa chama hicho
kwani ni sehemu ya mapambano na nguvu zinazowekwa katika kupambana na magonjwa
ya ndani ikiwemo magonjwa ya mfumo wa umeme wa moyo.
Dkt. Mwanaada ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya
ndani na mfumo wa upumuaji Hospitali ya Taifa Muhimbili alisema jitihada za
uanzishwaji wa chama hicho zinapaswa kuungwa mkono kwa lengo la kuwasaidia
wagonjwa kupata matibabu stahiki.
“Sisi kama chama cha magonjwa ya ndani tunaliunga mkono suala
hili na tuko hapa kutoa ushirikiano wowote unaohitajika kwaajili ya kupeleka
nguvu hizi mbele kwani tunatambua magonjwa haya hayajapewa kipaumbele japokuwa
yanasababisha vifo vingi katika jamii”, alisema Dkt. Mwanaada
Comments
Post a Comment