Upimaji na matibabu ya moyo bila malipo; Wanahabari kupewa kipaumbele
Baadhi ya wananchi waliofika Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) wakisubiri kupata huduma za upimaji na matibabu ya moyo zilizokuwa zinatolewa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa ALMC.
******************************************************************************************************************************************************************************************************
TAARIFA KWA UMMA
UPIMAJI NA MATIBABU YA MOYO BILA MALIPO KLINIKI YA JKCI KAWE WANAHABARI KUPEWA KIPAUMBELE
Wataalamu
wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji
Dkt. Peter Kisenge watatoa huduma za tiba mkoba zijulikanazo kwa jina la Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan Outreach Services kwa kufanya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo
kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam na
mikoa ya jirani.
Huduma hii itatolewa bila malipo kwa watoto na watu
wazima wakiwemo Waandishi wa Habari lengo likiwa ni kusogeza huduma za
kibingwa za matibabu ya moyo karibu zaidi na wananchi.
Matibabu haya yatatolewa tarehe 29-30/10/2024
kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni katika Kliniki ya JKCI Kawe
iliyopo Kawe jengo la Mkapa Health Plaza barabara ya
Tuari.
Kutakuwa na wataalamu wa lishe watakaotoa elimu
ya lishe bora itayayowapa wananchi uelewa wa kufuata mtindo bora wa
maisha na kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo yanayoweza
kuepukika kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.
Tunawaomba wananchi mjitokeze kwa wingi kupima afya zenu kujua kama mna matatizo ya moyo ili kuanza matibabu mapema kwa atakayegundulika kuwa mgonjwa.
Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa simu namba 0783922571 na 0680280007 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Kliniki ya Kawe.
“Afya ya Moyo Wako ni Jukumu Letu”.
Comments
Post a Comment