kambi maalumu ya upimaji na matibabu ya moyo mkoani Mwanza
Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Michael Lazaro akimpima shinikizo la damu mwananchi aliyetembelea banda la JKCI – Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato Kliniki ya moyo leo wakati wa maonesho ya 7 ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya bombambili Mkoani Geita.
*************************************************************************************************************************************************************************
TAARIFA KWA UMMA
KAMBI MAALUMU YA UPIMAJI NA MATIBABU
YA MOYO MKOANI MWANZA
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza (Sekou Toure) tutatoa
huduma za tiba mkoba zijulikanazo kwa jina la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
Outreach Services kwa kufanya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa
wananchi wa Mkoa wa Mwanza na mikoa ya jirani.
Upimaji huu utafanyika kwa watoto na watu
wazima tarehe 28/10/2024 - 01/11/2024 saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni
katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza (Sekou Toure) iliyopo Isamilo jijini
Mwanza.
Aidha kutakuwa na wataalamu wa lishe ambao
watatoa elimu ya lishe bora itakayowapa wananchi uelewa na kufuata mtindo bora
wa maisha utakaowasaidia kuepukana na magonjwa ya moyo ambayo ni moja ya
magonjwa yasiyoambukiza na yanaweza kuepukika kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.
Watakaogundulika kuwa na matatizo ya moyo
watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu hapo hapo au kupewa rufaa ya
kuja kutibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Upanga
jijini Dar es Salaam.
Tunawaomba
wananchi mjitokeze kwa wingi kupima afya zenu kujua kama mna matatizo ya moyo
ili kuanza matibabu mapema kwa atakayegundulika kuwa mgonjwa.
Kwa taarifa zaidi
wasiliana kwa simu namba 0738 153 160.
“Afya ya Moyo Wako ni Jukumu
Letu”.
Imetolewa na:
Anna Nkinda
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na
Mawasiliano
Comments
Post a Comment