Mtoto Witness awasili JKCI kwaajili ya Matibabu

Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jimmy Mchalange akimpokea mtoto Witness Lukumay aliyegundulika kuwa na tatizo la moyo wakati wa kambi maalumu ya upimaji na matibabu ya moyo iliyofanyika Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) wiki iliyopita baada ya mtoto huyo kuwasili JKCI leo kwaajili ya matibabu. Mtoto huyo anayepatiwa matibabu bila gharama amesafirishwa kutoka Arusha na gari la Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI. 

Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jackline Mwaipopo akimpeleka mtoto Witness Lukumay kufanyiwa vipimo baada ya mtoto huyo kugundulika kuwa na tatizo la moyo wakati wa kambi maalumu ya upimaji na matibabu ya moyo iliyofanyika Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) wiki iliyopita na kuwasili leo JKCI kwaajili ya matibabu.

Mama wa mtoto aliyegundulika kuwa na tatizo la moyo wakati wa kambi maalumu ya upimaji na matibabu ya moyo iliyofanyika Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) wiki iliyopita Witness Lukumay akimsajili mtoto huyo baada ya kuwasili Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwaajili ya matibabu. Mtoto huyo anayepatiwa matibabu bila gharama amesafirishwa kutoka Arusha na gari la Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI.

Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jackline Mwaipopo akimpima mtoto Witness Lukumay joto la mwili baada ya mtoto huyo kugundulika kuwa na tatizo la moyo wakati wa kambi maalumu ya upimaji na matibabu ya moyo iliyofanyika Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) wiki iliyopita na kupewa rufaa kufika JKCI leo kwaajili ya matibabu.

Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Zubeida Hussein akimfanyia kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) mtoto Witness Lukumay aliyegundulika kuwa na tatizo la moyo wakati wa kambi maalumu ya upimaji na matibabu ya moyo iliyofanyika Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) wiki iliyopita na kupewa rufaa kufika JKCI leo kwaajili ya matibabu.

Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jimmy Mchalange akizungumza na mama wa mtoto Witness Lukumay aliyegundulika kuwa na tatizo la moyo wakati wa kambi maalumu ya upimaji na matibabu ya moyo iliyofanyika Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) wiki iliyopita na kupewa rufaa kufika JKCI leo kwaajili ya matibabu. Mtoto huyo anayepatiwa matibabu bila gharama amesafirishwa kutoka Arusha na gari la Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI.

Picha na: JKCI

 ***********************************************************************************************************************************

Comments

Popular posts from this blog

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yapata tuzo ya taasisi ambayo imetoa mchango wa kipekee kiuchumi na kijamii katika kuleta matokeo makubwa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024

Maabara ya JKCI yapata ithibati ya kimataifa (ISO 15189:2012)