Dkt. Kisenge: Elimu mliyoipata iokoe maisha ya wagonjwa wa dharura na mahututi
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wahitimu wa mafunzo bobezi ya matibabu ya
moyo katika program ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa mahututi na dharura wakati
wa hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika leo katika Taasisi hiyo iliyopo jijini
Dar es Salaam. Mafunzo hayo yanafanywa na JKCI kwakushirikiana na Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam (UDSM).
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
anayeshughulikia Tafiti Prof. Nelson Boniface akielezea namna mafunzo bobezi ya
matibabu ya moyo katika program ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa mahututi na
dharura yanavyofanyika wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wahitimu wa mafunzo
hayo iliyofanyika leo jijini Dar es
Salaam. Mafunzo hayo yanafanywa na JKCI kwakushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam (UDSM).
Mkuu wa Kitengo cha Mafunzo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Dkt. Khuzeima Khanbhai akiwapongeza wahitimu wa mafunzo bobezi ya
matibabu ya moyo katika program ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa mahututi na
dharura wakati wa hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika leo katika Taasisi hiyo
iliyopo jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo yanafanywa na JKCI kwakushirikiana
na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Wahitimu wa mafunzo bobezi ya matibabu ya moyo katika program
ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa mahututi na dharura wakifuatilia yaliyokuwa
yakiendelea wakati wa hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika leo katika Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo
yanafanywa na JKCI kwakushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Mhitimu wa mafunzo bobezi ya matibabu ya moyo katika program
ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa mahututi na dharura Alphonce John akipokea
cheti cha kuhitimu mafunzo hayo wakati wa hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika
leo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mafunzo hayo yanafanywa na JKCI kwakushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM).
Mhitimu wa mafunzo bobezi ya matibabu ya moyo katika program
ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa mahututi na dharura Anithar Kanick akipokea cheti cha kuhitimu mafunzo hayo
wakati wa hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika leo katika Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) iliyopo jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo yanafanywa na JKCI
kwakushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Mhitimu wa mafunzo bobezi ya matibabu ya moyo katika program ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa mahututi na dharura Leodgard Elias akitoa neno la shukrani wakati wa hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika leo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo yanafanywa na JKCI kwakushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa UDSM, JKCI na
wahitimu mafunzo bobezi ya matibabu ya moyo katika program ya jinsi ya
kuwahudumia wagonjwa mahututi na dharura wakati wa hafla fupi ya kuwaaga
wahitimu hao iliyofanyika leo katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mafunzo hayo yanafanywa na JKCI kwakushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM).
Na: JKCI
*********************************************************************************************************
Wahitimu wa mafunzo bobezi ya matibabu ya moyo katika program
ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa mahututi na dharura wametakiwa kutumia elimu
waliyoipata kuokoa maisha ya wagonjwa hao wanaowategemea wakati wa dharura.
Rai hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge wakati wa mahafali ya kwanza ya
program hiyo inayofanywa na JKCI kwakushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM).
Dkt. Kisenge alisema program hiyo ya miezi sita imekuwa
ikifanywa na JKCI kipindi cha nyuma hadi hapo ndoto ya kushirikiana na UDSM
ilivyotimia ambapo wahitimu hao wamekuwa wahitimu wakwanza kumaliza mafunzo
hayo tangu ushirikiano huo ulivyoanza mwezi machi mwaka huu.
“Kwetu sisi hii ni historia kubwa kwa taasisi, safari yetu
ilianza tangu mwaka 2015 na leo tunaandika historia ya kuungana na UDSM chuo
chenye uwezo mkubwa katika kutoa mafunzo, popote mtakapoenda mtakuwa wa mfano
kupitia mafunzo haya mliyoyapata kwetu”, alisema Dkt. Kisenge
Dkt. Kisenge alisema JKCI na UDSM wataendelea kutengeneza
misingi mizuri katika kutoa mafunzo ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura na
mahututi kuboresha huduma kupitia wataalamu wa afya waliopo Hospitali za
Wilaya, Mikoa na Rufaa.
“Leo wanahitimu wauguzi 11 wakiwemo wanne kutoka nchini Zambia
na saba kutoka Tanzania ambapo wawili wanatoka hospitali ya jeshi Arusha, mmoja
hospitlia ya rufaa ya mkoa wa Temeke, mmoja hospitali ya Kigamboni, mmoja JKCI,
mmoja kutoka Hospitali ya Lugalo na mmoja amepata ajira hivi karibuni mkoani
Arusha”, alisema Dkt. Kisenge
Dkt. Kisenge alisema ushirikiano wa JKCI na UDSM umeweza
kutengeneza program nyingine za mafunzo ikiwemo udaktari bingwa wa masuala ya
upasuaji wa moyo kwa njia ya tundu dogo ambazo zitakuwa za kwanza Afrika
Mashariki na Kati kutolewa hapa nchini.
Kwa upande wake Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam anayeshughulikia Tafiti Prof. Nelson Boniface alisema JKCI inatekeleza
jukumu la UDSM la kuendeleza maaarifa na mafunzo kwa kufanya tafiti na kutoa
ujuzi kwa wataalamu wa afya.
Prof. Nelson aliwataka wahitimu hao kuishukuru JKCI kwa kutoa
fursa kwao kuweza kupata ujuzi na kupewa nafasi ya kutumia vifaa tiba vya
kisasa wakati wa mfunzo kwa vitendo.
“Ninayo furaha kushuhudia mahafali ya kwanza ya ushirikiano
wetu na JKCI, maarifa mliyoyapata kwetu mkayatumie vizuri muweze kukabiliana na
maendeleo ya sayansi na teknolojia”, alisema Prof. Nelson
Naye Afisa Uuguzi aliyemaliza mafunzo hayo Cecilia Mjungu
aliwashukuru wakufunzi waliohusika kutoa mafunzo ambayo yameweza kuwabadilisha
na kuweza kukabiliana na changamoto wakati wakutoa huduma kwa wagonjwa.
Cecilia alisema baada ya kukutana na wauguzi kutoka nchini
Zambia na kubadilishana nao ujuzi ameiona Tanzania kuwa na uwezo mkubwa katika
kutoa huduma kwa wagonjwa mahututi na wadharura uwezo ambao wauguzi wakipitia
mafunzo hayo wanaweza kufanya kazi nchi yoyote.
“Nawashauri na wauguzi wenzangu ambao bado hawajapata mafunzo
haya wajitokeze kuendeleza ujuzi, sisi leo tupo tayari kupambania maisha ya mgonjwa
aliyopo katika hatari ya kupoteza uhai wake”, alisema Cecilia.
Comments
Post a Comment