Upimaji na matibabu ya moyo bila malipo tarehe 12/10/2024


Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Michael Lazaro akimpima shinikizo la damu mwananchi aliyetembelea banda la JKCI – Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato Kliniki ya moyo leo wakati wa maonesho ya 7 ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika viwanja vya bombambili Mkoani Geita.

********************************************************************************************************************************************************************************************************

TAARIFA KWA UMMA

UPIMAJI NA MATIBABU YA MOYO BILA MALIPO TAREHE 12/10/2024

Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa mteja tarehe 07-11 Oktoba 2024 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) itatoa huduma ya upimaji na matibabu ya moyo kwa wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani  bila malipo yoyote yale.

Upimaji huu utafanyika kwa watoto na watu wazima siku ya jumamosi ya tarehe 12/10/2024  kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Upanga, JKCI Dar Group iliyopo TAZARA na JKCI Kliniki ya Kawe iliyopo Kawe jengo la Mkapa Health Plaza barabara ya Tuari.

Kutakuwa na wataalamu wa lishe watakaotoa elimu ya lishe bora itayayowapa  wananchi uelewa wa  kufuata mtindo bora wa maisha na kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo yanayoweza kuepukika kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.

 

Tunawaomba wananchi mjitokeze kwa wingi kupima afya zenu kujua kama mna matatizo ya moyo ili kuanza matibabu mapema kwa atakayegundulika kuwa mgonjwa.

Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa simu namba  0788308999 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Upanga, 0674179036 JKCI Dar Group na 0680280007 JKCI  Kliniki ya Kawe.

“Afya ya Moyo Wako ni Jukumu Letu”.

 

Imetolewa na :


Anna Nkinda

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano

 

Comments

Popular posts from this blog

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yapata tuzo ya taasisi ambayo imetoa mchango wa kipekee kiuchumi na kijamii katika kuleta matokeo makubwa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024

Maabara ya JKCI yapata ithibati ya kimataifa (ISO 15189:2012)