JKCI na Yanga kushirikiana kufikisha elimu ya magonjwa ya moyo katika jamii
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Mpira wa Miguu ya Yanga Andre Mtine wakibadilishana hati ya mkataba wa ushirikiano kati ya JKCI na Klabu ya Yanga baada ya kusaini hati hizo leo katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam
Afisa Mtendaji wa Mkuu wa Klabu ya Mpira wa Miguu ya Yanga Andre Mtine akimpatia jezi ya klabu hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) mara baada ya kusaini hati ya mkataba wa ushirikiano kati ya JKCI na Klabu ya Yanga leo katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt.
Peter Kisenge akimuonesha moja ya wodi za VIP Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya
Mpira wa Miguu ya Yanga Andre Mtine mara baada ya kusaini hati ya mkataba wa
ushirikiano kati ya JKCI na Klabu ya Yanga leo katika Taasisi hiyo iliyopo
jijini Dar es Salaam
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naiz Majani akimuelezea hali ilivyo katika wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Mpira wa Miguu ya Yanga Andre Mtine mara baada ya kusaini hati ya mkataba wa ushirikiano kati ya JKCI na Klabu ya Yanga leo katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kusaini hati ya mkataba wa ushirikiano kati ya JKCI na Klabu ya mpira wa miguu ya Yanga leo katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam
Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Mpira wa Miguu ya Yanga Andre Mtine akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kusaini hati ya mkataba wa ushirikiano kati ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Klabu ya mpira wa miguu ya Yanga leo katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt.
Peter Kisenge akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa klabu ya mpira wa
miguu ya Yanga na wafanyakazi wa JKCI mara baada ya kusaini hati ya mkataba wa
ushirikiano kati ya JKCI na Klabu ya Yanga leo katika Taasisi hiyo iliyopo
jijini Dar es Salaam
Baadhi ya waandishi wa habari wakichukua matikio ya picha wakati wa kusaini hati ya mkataba wa ushirikiano kati ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Klabu ya Mpira wa Miguu ya Yanga leo katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam
Picha na JKCI
******************************************************************************************************************
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Klabu ya Mpira wa
Miguu ya Yanga zimesaini hati ya mkataba wa ushirikiano katika utendaji wa kazi
na kuielimisha jamii kuhusu magonjwa moyo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam mara
baada ya kusaini mkataba huo Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Dkt. Peter Kisenge
alisema JKCI ndio taasisi pekee inayotoa huduma za upasuaji wa moyo nchini na ya
tatu kwa ukubwa Barani Afrika katika kutoa huduma za matibabu ya moyo pamoja na
upasuaji wa moyo.
Pamoja na kusaini mkataba huo Dkt. Kisenge pia ametoa ofa kwa
mashabiki wa timu hiyo wenye kadi za uanachama kufanyiwa uchunguzi na matibabu
ya moyo kwa punguzo la asilimia 20 katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI).
“JKCI imekuwa ikitoa huduma kwa wagonjwa zaidi ya 900 kwa
siku na kufanya upasuaji wa moyo kwa wagonjwa 700 kwa mwaka ambapo asilimia 20
ya upasuaji wa huo unaofanyika kwa watoto wadogo ambao wengi wao wanatoka
katika familia masikini zisizokuwa na uwezo wa kugharama matibabu ya moyo”,
alisema Dkt. Kisenge
Dkt. Kisenge alisema JKCI kuungana na klabu ya Yanga kuna
faida kwani kupitia klabu hiyo JKCI itafahamika zaidi ndani na nje ya nchi
lakini pia kutoa nafasi kwa wachezaji wa timu hiyo kufanyiwa uchunguzi wa
magonjwa ya moyo.
“Serikali yetu inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inachangia asilimia 70 katika matibabu
ya watoto wetu na asilimia 20 inayobaki tunasema kuwa hatutaki mtoto hata mmoja
anayefika JKCI akose matibabu ndio maana tunaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali
ikiwemo klabu ya Yanga”, alisema Dkt. Kisenge
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Yanga Andre Mtine alisema JKCI imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kuokoa maisha ya watanzania wanaohitaji huduma za matibabu ya moyo hivyo Klabu ya Yanga ikaamua kuchukua jukumu la kuwa sehemu ya JKCI kuhamasisha jamii kujitokeza kupima na kuitangaza JKCI ndani na nje ya nchi.
“Kila mtu anajua yakuwa taifa lililo na afya bora ni taifa
lililo na furaha hivyo kutokana na sababu hiyo ndio maana sisi Yanga tumeamua
kuungana na JKCI kuhamasisha jamii kuwa na afya bora”, alisema Andre
Andre alitoa wito kwa wanachama wa klabu ya Yanga kuhakikisha
wanapata kadi za uanachama ili waweze kupata ofa iliyotolewa na JKCI ya kupatiwa
huduma za kibingwa za uchunguzi na matibabu ya moyo.
“Klabu ya Yanga itashiriki katika usiku wa dinner gala unaoandaliwa na Taasisi kwa
lengo la kuchangia matibabu ya watoto wanaotibiwa JKCI ili nasi tuwe sehemu ya
kujenga Taifa lililo na furaha”, alisema Andre
Naye daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naiz Majani alisema uelewa wa magonjwa ya moyo
katika jamii umekuwa mkubwa na kuifanya jamii kutafuta matibabu pale tu
inapoona dalili za magonjwa hayo.
“Wodi yetu ya watoto ina uwezo wa kulaza watoto 23 lakini
kutokana na uhitaji kuwa mkubwa leo hii tuna watoto 48 ambao wengine tumewalaza
katika wodi za watu wazima”, alisema Dkt. Naiz
Dkt. Naiz alisema kupitia wadau mbalimbali watoto wengi
wamekuwa wakipatiwa huduma za upasuaji wa moyo lakini kutokana na tatizo hilo
kuwa kubwa kila wanapozaliwa watoto 100 kati ya mtoto 1 hadi 2 huzaliwa na
tatizo la moyo hivyo kuendelea kufanya idadi ya watoto wanaosubiria upasuaji wa
moyo kutopungua.
Comments
Post a Comment