JKCI yamshukuru mfanyabiashara maarufu Shija Tajiri Vunjabei
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akipokea zawadi ya water dispenser kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Vunjabei vyombo mfanyabiashara Shija Tajiri Vunjabei ambayo itatumika kwa wagonjwa wa taasisi hiyo. Kampuni ya Vunjabei vyombo ilitembelea taasisi hiyo leo na kutoa zawadi za vyombo kwa wafanyakazi wa JKCI kwaajili ya kutambua na kuthamini huduma wanayoitoa ya kuokoa maisha ya wagonjwa wenye matatizo ya moyo.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Ivon Mushi akipokea zawadi ya vikombe vya chai kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Vunjabei vyombo mfanyabiashara Shija Tajiri Vunjabei alipofika katika taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam na kutoa zawadi za vyombo kwa wafanyakazi wa JKCI kwaajili ya kutambua na kuthamini huduma wanayoitoa ya kuokoa maisha ya wagonjwa wenye matatizo ya moyo.
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Engerasia Kifai akipokea zawadi ya multi cooker kutoka kwa mfanyakazi wa Kampuni ya Vunjabei vyombo walipofika katika taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam na kutoa zawadi za vyombo kwa wafanyakazi wa JKCI kwaajili ya kutambua na kuthamini huduma wanayoitoa ya kuokoa maisha ya wagonjwa wenye matatizo ya moyo.
Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) CPA. Illuminata Marimbo akitoka kupokea zawadi ya seti ya glass na jagi la maji kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Vunjabei vyombo mfanyabiashara Shija Tajiri Vunjabei alipofika katika taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam na kutoa zawadi za vyombo kwa wafanyakazi wa JKCI kwaajili ya kutambua na kuthamini huduma wanayoitoa ya kuokoa maisha ya wagonjwa wenye matatizo ya moyo.
************************************************************************************************************************************************************************************
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge ameishukuru kampuni ya Vunjabei vyombo kwa kutoa zawadi za vyombo vya nyumbani kwa wafanyakazi wa taasisi hiyo.
Akishukuru kwa niaba ya wafanyakazi wa JKCI mara baada ya kupokea zawadi hizo Dkt.Kisenge alisema muda mwingi wanakuwa na kazi nyingi za kuwahudumia wagonjwa na hivyo kukosa muda wa kwenda kununua vyombo madukani lakini kutokana na zawadi za vyombo walizopewa pamoja na vingine wakatavyonunua kutoka kwa kampuni hiyo kutawapunguzia muda wa kuvifuata madukani.
“Nitumie nafasi hii kumshukuru mfanyabiashara maarufu Shija Tajiri Vunjabeikwa kutambua kazi inayofanywa na wataalamu wetu ya kuwatibu wagonjwa wenye matatizo ya moyo na kuamua kuja kutupa zawadi za vyombo, tunawaomba muendelee na moyo huo huo wa kuwajali wafanyakazi wetu ili nao wafurahi na kuona kuna watu wanathamini na kutambua kazi wanayoifanya”,alisema Dkt. Kisenge.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Vunjabei vyombo
mfanyabiashara Shija Tajiri Vunjabei alisema lengo la kufika katika taasisi
hiyo ni kuwapongeza wafanyakazi wa JKCI na kutambua mchango wao wa kazi wanayoifanya
ya kuokoa maisha ya watu wenye matatizo ya moyo.
“Wafanyakazi wengi wa Serikali wanakosa muda wa kutosha wa kwenda kufanya manunuzi hivyo tupo hapa kwanza kuwapa zawadi ili kuwapa motisha ya kufanya kazi kwa bidii zaidi lakini pia kuwauzia vyombo na vifaa vingine vya ndani kwa bei naafuu na zoezi hili litakuwa endelevu”, alisema Neema.
Nao wafanyakazi wa taasisi hiyo waliopata zawadi za vyombo walishukuru kwa zawadi walizopewa na kusema kuwa zimewapa hamasa ya kufanya kazi kwa bidii zaidi kwani wameona ni jinsi gani jamii inatambua kazi wanazozifanya.
“Leo hii nimepewa zawadi ya multi cooker pia nitanunua
vyombo vingine ambavyo sina nyumbani, kununua vyombo hapa kumeokoa muda wangu wa
kuvifuata dukani pia bei ni rahisi nitaokoa fedha yangu”, alishukuru Anna
Emmanuel.
Comments
Post a Comment