JKCI – Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato kliniki ya moyo yaibuka mshindi wa kwanza Taasisi inayotoa huduma za afya maonesho ya madini Geita
Waziri wa Madini Mhe. Antony Mavunde akimpatia tuzo ya mshindi wa kwanza Taasisi zinazotoa huduma za afya maonesho ya 7 ya teknolojia ya madini Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge leo katika viwanja vya Bombambili Mkoani Geita.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge akimuelezea Waziri wa Madini Mhe. Antony Mavunde namna kifaa
maalumu kijulikanacho kwa jina la DOZEE kinachotumika kufuatilia maendeleo ya
mgonjwa anayetibiwa akiwa nyumbani kinavyofanya kazi alipotembelea banda la
JKCI – Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato kliniki ya moyo wakati wa maonesho ya
7 ya teknolojia ya madini yanayofanyika katika viwanja vya Bombambili mkoani
Geita.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wananchi wanaosubiri kupata huduma katika banda
la JKCI – Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato kliniki ya moyo wakati wa maonesho
ya 7 ya teknolojia ya madini yanayofanyika katika viwanja vya Bombambili mkoani
Geita.
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Dkt. Salehe Mwinchete akitoa elimu ya namna ya kujikinga na
magonjwa yasiyoambukiza kwa wananchi wanaosubiri kupata huduma katika banda la
JKCI – Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato kliniki ya moyo wakati wa maonesho ya
7 ya teknolojia ya madini yanayofanyika katika viwanja vya Bombambili mkoani
Geita.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Kisenge akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa JKCI na wenzao wa
Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato kliniki ya moyo baada ya kupokea tuzo ya
mshindi wa kwanza Taasisi zinazotoa huduma za afya maonesho ya 7 ya teknolojia
ya madini leo Mkoani Geita.
Na: JKCI
********************************************************************************************************
Comments
Post a Comment