Posts

Wafundishwa jinsi ya kufanya kipimo cha ECHO

Image
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Engerasia Kifai akiwafundisha wataalamu kutoka Hospitali mbalimbali namna ya kufanya kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) wakati wa mafunzo ya wiki mbili kwa wataalamu hao. Jumla ya wataalamu 40 kutoka Hospitali mbalimbali nchini na mmoja kutoka nchini Kenya wanashiriki mafunzo hayo. Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Johnstone Kayandabila akiwafundisha wataalamu kutoka Hospitali mbalimbali namna ya kufanya kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) wakati wa mafunzo ya wiki mbili yanayoendelea katika Taasisi hiyo. Jumla ya wataalamu 40 kutoka Hospitali mbalimbali nchini na mmoja kutoka nchini Kenya wanashiriki mafunzo hayo. Mhadhiri mwandamizi Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof. Pilly Chillo akiwafundisha wataalamu kutoka Hospitali mbalimbali nchini namna ya kufanya kipim...

JKCI yawafuata wagonjwa majumbani

Image

Pata huduma ya matibabu ya moyo kwa njia ya mtandao

Image

Kwa mara ya kwanza upasuaji wa kurekebisha valvu ya moyo wafanyika kwa mtu mzima

Image
Wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimfanyia mgonjwa upasuaji mkubwa wa moyo wa kurekebisha Valvu. ************************************************************************************************************* Kwa mara ya kwanza upasuaji wa kurekebisha valvu za moyo kwa watu wazima umefanyika kwa mgonjwa ambaye valvu yake ya moyo ya upande wa kushoto ilikuwa ikivujisha damu (severe mitral regurgitation). Upasuaji huo umefanywa hivi karibuni na madaktari bingwa wa upasuajia wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na mwenzao kutoka Serikali ya Watu wa China. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi  Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Williams Ramadhan alisema upasuaji wa kurekebisha valvu za moyo umekuwa ukifanyika kwa watoto wenye shida za valvu lakini kwa watu wazima mgonjwa huyo amekuwa wa kwanza kurekebishiwa valvu yake kwani wagonjwa wengine wamekuwa wakiwekew...

Wanafunzi UDSM watoa zawadi kwa watoto wenye matatizo ya moyo na kuchangia damu chupa 14

Image
Mwanachuo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)   mwaka wa Tatu anayesomea    Biashara upande wa Masoko Belinda Mlay akimkabidhi zawadi mama wa mtoto aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya matibabu ya moyo. Wanachuo hao wa UDSM walitembelea JKCI hivi karibuni kwaajili ya kutoa zawadi kwa watoto pamoja na kuchangia damu. Mwanachuo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka wa Tatu anayesomea Biashara upande wa Masoko Giveness Kitale akimkabidhi zawadi mama wa mtoto aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya matibabu ya moyo. Wanachuo hao wa UDSM walitembelea JKCI hivi karibuni kwaajili ya kutoa zawadi kwa watoto pamoja na kuchangia damu. Mwanachuo wa mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) anayesomea Biashara upande wa Masoko George Temba akimkabdhi zawadi za watoto waliolazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Afisa Muuguzi Msaidizi Grace Sanga. Wanachuo hao wa UDSM walitembelea JKCI hivi...

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa: Fanyeni mazoezi kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza

Image
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiwaongaza wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam katika matembezi ya pamoja aliyoyazindua rasmi leo kwaajili ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza. Matembezi hayo yameanzia katika viwanja vya Coco beach kuelekea daraja la Tanzanite hadi makutano ya barabara ya hospitali ya Aga khan kuelekea Taasisi ya Ocean Road na kurudi Coco beach. Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika matembezi ya pamoja yaliyozinduliwa leo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kwaajili ya kupambana na magonjwa yasiyoambukiza. Matembezi hayo yameanzia katika viwanja vya Coco beach kuelekea daraja la Tanzanite hadi makutano ya barabara ya hospitali ya Aga khan kuelekea Taasisi ya Ocean Road na kurudi Coco beach. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wengine wakifanya mazoezi ya viungo mara baada ya kumaliza matembezi ya pamoja aliyoyazindua l...

Sierra Leone wajifunza JKCI walivyopiga hatua kubwa katika matibabu ya moyo barani Afrika

Image
Kaimu Mkuu wa Hospitali ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dar Group Dkt. Tulizo Shemu akiwaeleza wageni kutoka nchini Sierra Leonne huduma zinazotolewa katika kliniki na wodi za watu maalumu na wagonjwa kutoka nje ya nchi wakati walipotembelea Taasisi hiyo leo kwaajili ya kuona   huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo   pamoja na kujifunza namna ambavyo JKCI imepiga hatua kubwa katika   matibabu ya moyo barani Afrika. Mganga Mkuu wa Serikali ya Sierra Leonne Dkt. Sartie Mohamed Kenneth akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara ya wajumbe kutoka nchini humo ambao walitembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwaajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa pamoja na kujifunza namna ambavyo JKCI imepiga hatua kubwa katika matibabu ya moyo barani Afrika. Msimamizi wa wodi ya watoto ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Afisa Uuguzi Theresia Tarimo  akiwaeleza wageni  kutoka nchini Sierra Leonne huduma wanazozipata ...