Waliofanyiwa upasuaji wa moyo waishukuru Serikali kwa kuboresha huduma za matibabu ya moyo nchini

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akitoa cheti cha shukrani kwa Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu Bashir Nyangasa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano cha Taasisi hiyo Anna Nkinda kilichotolewa na Jumuia ya Moyo ni Uhai kwa kutambua mchango wa JKCI wa kuwapatia huduma za matibabu ya kibingwa ya moyo. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wanachama wa Jumuia ya Moyo ni Uhai ambao ni wagonjwa waliofanyiwa na wanaosubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo wakati wa mkutano wao mkuu wa kwanza uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. Jumuia hiyo ina wanachama zaidi ya 300 waliofanyiwa upasuaji wako zaidi ya 140 na wanaosubiri kufanyiwa upasuaji wako zaidi ya 160. Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Bashir Nyangasa akitoa elimu ya lishe ...