JKCI yapongezwa kwa kuanza kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo akiweka jiwe la msingi la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) tawi la Temeke kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mwigulu Nchemba jana wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi iliyofanyika katika Taasisi hiyo tawi la Dar Group lililopo Tazara jijini Dar es Salaam. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Naibu Waziri wa Afya Dkt. Florence Samizi na viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) tawi la Temeke iliyofanyika jana katika Hospitali ya JKCI Dar Group iliyopo Tazara jijini Dar es Salaam. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Hassan Mahmoud Mshinda wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi la Taasis...