Idara zilizotoa huduma bora kwa wateja zapongezwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi hiyo wakati wa kikao cha kupitia taarifa ya ukaguzi wa ndani wa huduma zinazotolewa na Taasisi hiyo kwa mwezi Oktoba hadi Desemba 2022 kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akikabidhi cheti cha mshindi wa kwanza katika kutoa huduma bora kwa wateja kiongozi wa chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) Afisa Muuguzi Lucia Kabeya wakati wa kikao cha wafanyakazi wa Taasisi hiyo kupitia taarifa ya ukaguzi wa ndani wa huduma zinazotolewa na Taasisi hiyo jana jijini Dar es Salaam. Kitengo cha ICU kimeongoza kwa kutoa huduma bora kwa kipindi cha mwezi Oktoba hadi Desemba 2022. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimkabidhi cheti cha mshindi wa pili katika kutoa huduma bora kwa wateja Mkuu wa Idara ya Famasia Wellu Kaali wakati wa kikao ch...