Upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo wilayani Siha

Afisa Lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Husna Faraji akitoa elimu ya lishe bora kwa wananchi waliofika JKCI hospitali ya Dar Group kwaajili ya upimaji na matibabu ya moyo wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo Duniani yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. ************************************************************************************************************************************* ************************************************************ Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Hospiitali ya Wilaya ya Siha iliyopo mkoani Kilimanjaro watatoa huduma za tiba mkoba ijulikanayo kwa jina la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services kwa kufanya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wananchi wa Wilaya ya Siha na Wilaya jirani. Upimaji huu ambao utaenda sambamba na ushiriki wa JKCI katika mbio za Siha Marathon utafanyika kwa watoto na watu wazima kuanzia tarehe 18/12/2023 hadi tarehe 22/12/2023 saa m...