JKCI kuokoa milioni 500 wagonjwa wa moyo 15 kutibiwa nchini
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu kambi maalumu ya upasuaji wa moyo inayofanywa na wataalamu wa afya wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Cardiostart International la nchini Marekani. Kambi hiyo maalumu ya siku tano imeanza leo kwa mafunzo ya siku moja kwa wataalamu wa afya wa JKCI. Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto na watu wazima kutoka Shirika la Cardiostart International la nchini Marekani Prof. Aubyn Marath akielezea mafanikio ya ushirikiano baina na JKCI na Cardiostart International wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu kambi maalumu ya siku tano inayofanywa na wataalamu hao katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu kwa watu wazima kutoka Shirika la Cardiostart International la nchini Marekani Prof. Gustavo Knop akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu kambi ...