Kateni bima za afya kumudu gharama za matibabu – Prof.Janabi
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimpima shinikizo la damu (BP) mwananchi aliyetembelea banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya kufanya vipimo vya magonjwa ya moyo na kisukari wakati wa maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa. Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agnes Kuhenga akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Taasisi hiyo lililopo katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa. Mteknolojia wa maabara wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jordan Megabe akimchukuwa kipimo cha damu mwananchi aliyetembelea banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya kumfanyia vipimo vya kuchunguza figo, ini na kiwango cha mafuta mwilini wakati wa Maonesho ya 46 ya Biashara ya K...