Waziri Ummy: Tafuteni eneo kubwa la matibabu ya moyo
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akizindua bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo jijini Dar es Salaam. Daktari wa wagonjwa waliolazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Iddi Makapu akiwaeleza wajumbe wa bodi ya wadhamini ya Taasisi hiyo huduma zinazotolewa katika chumba hicho walipotembelea ICU kabla ya uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika leo katika Ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo. Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza na wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) alipofika katika taasisi hiyo leo jijini Dar ea Salaam kwaajili ya kuzindua Bodi ya Wadhamini ya JKCI. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwaeleza wajumbe wa bodi ya wadhamini ya Taasisi hiyo huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa kwa watoto wanaolazwa katika Taasisi hiyo wakati wajumbe hao walitembelea wodi ya watoto ya JKCI. Daktari bingwa wa upas...