Posts

Dkt. Mpango: Tanzania yapiga hatua matibabu ya moyo

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akipokea zawadi kutoka kwa kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Asha Izina wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa magonjwa ya moyo katika ukumbi wa Golden Tulip uliopo mjini Zanzibar. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na wataalamu wa afya nchini walioshiriki katika Mkutano wa kimataifa wa magonjwa ya moyo leo wakati wa ufunguzi wa mkutano huo katika ukumbi wa Golden Tulip uliopo mjini Zanzibar. Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa kimataifa wa magonjwa ya moyo leo katika Ukumbi wa Golden Tulip uliopo mjini Zanzibar. Baadhi ya washiriki wa mkutano wa kimataifa wa magonjwa ya moyo wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa katika mkutano huo leo mjini Zanzibar.  ******************************************************************************************************************...

Mkutano wa kimataifa wa magonjwa ya moyo kufanyika Zanzibar

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kongamano la wataalamu wa afya leo kabla ya mkutano wa magonjwa ya moyo utakaofanyika kesho katika Hoteli ya Golden Tulip iliyopo Zanzibar. Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Godwin Sharau akielezea mada zitakazotolewa katika mkutano wa magonjwa ya moyo utakaofanyika kesho katika Hoteli ya Golden Tulip iliyopo Zanzibar. Wataalamu wa afya kutoka Hospitali mbalimbali nchini wakifanya mazoezi kwa vitendo ya namna ya kuunganisha mishipa ya damu wakati wa kongamano leo kabla ya mkutano wa magonjwa ya moyo utakaofanyika kesho katika Hoteli ya Golden Tulip iliyopo Zanzibar Wataalamu wa afya kutoka Hospitali mbalimbali nchini wakifanya mazoezi kwa vitendo ya namna ya kumhudumia mgonjwa wa dharura wakati wa kongamano leo kabla ya mkutano wa magonjwa ya moyo utakaofanyika kesho katika Hoteli ya Golden Tulip iliyopo Zanzib...

Madaktari wa China wapokelewa JKCI

Image
Mkurugenzi wa Upasuaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angela Muhozya akizungumza na wataalamu wa afya kutoka Serikali ya Watu wa China walivyowasili katika Taasisi hiyo hivi karibuni kwaajili ya kushirikiana na wenzao wa JKCI kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa wagonjwa wanaotibiwa na Taasisi hiyo. Jumla ya wataalamu wa afya watatu wanatarajia kufanya kazi JKCI kwa kipindi cha miaka miwili.  Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Tiba Asilia na Tiba Mbadala   na mratibu wa ushirikiano wa kimataifa kutoka Wizara ya Afya Dkt. Liggyle Vumilia akiwatambulisha wataalamu wa afya kutoka Serikali ya Watu wa China watakaofanya kazi JKCI walipowasili katika taasisi hiyo hivi karibuni. Jumla ya wataalamu wa afya watatu wanatarajia kufanya kazi JKCI kwa kipindi cha miaka miwili.  

JKCI kushirikiana na Misri kuboresha matibabu ya moyo nchini

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wadau kutoka Kampuni ya STERI CARE iliyopo nchini Misri walipofika JKCI jana kwaajili ya kuangalia maeneo ambayo taasisi hiyo itashirikiana na kampuni hiyo kuboresha upatikanaji wa vifaa tiba na ujuzi katika kutoa huduma za matibabu ya moyo.  Baadhi ya wawakilishi kutoka Kampuni ya STERI CARE iliyopo nchini Misri wakifuatilia wakati wa kikao na uongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kujadili maeneo yakushirikiana kuboresha upatikanaji wa vifaa tiba na ujuzi katika kutoa huduma za matibabu ya moyo jana jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiwa katika picha ya pamoja na wadau kutoka Kampuni ya STERI CARE iliyopo nchini Misri baada ya kikao cha kuangalia maeneo ya ushirikiano jana katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. Na: JKCI *********************************************************************...

China kuleta vifaa tiba nchini

Image
Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel akimkaribisha Naibu Waziri Mkuu wa Serikali ya Watu wa China Mhe. Liu Guozhong alipofanya ziara katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo kuona huduma zinazotolewa.  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimuelezea mafanikio ya Taasisi hiyo tangu kuanzishwa kwake Naibu Waziri Mkuu wa Serikali ya Watu wa China Mhe. Liu Guozhong alipofanya ziara katika Taasisi hiyo leo kuona huduma zinazotolewa. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimuelezea huduma zinazotolewa katika chumba cha upasuaji wa tundu dogo (CathLab) Naibu Waziri Mkuu wa Serikali ya Watu wa China Mhe. Liu Guozhong alipofanya ziara katika Taasisi hiyo leo kuona huduma zinazotolewa. Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri Mkuu wa Serikali ya Watu wa China Mhe. Liu Guozhong na viongozi wengine wa Serikali mara baada ya ziara ya Naibu Wazir...

JKCI yafanya upasuaji wa moyo kwa watoto saba wa Zambia

Image
Madaktari wa Usingizi na Wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya Taifa ya Moyo ya nchini Zambia wakimlaza mtoto kwaajili ya kufanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi ya matibabu iliyomalizika jana nchini Zambia. Kambi hiyo ya siku tatu na nusu imewezeshwa na Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) la nchini Israel. Wataalamu wa afya wanaofanya kazi katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya Taifa ya Moyo ya nchini Zambia wakijaza fomu ya maendeleo ya mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi ya matibabu iliyomalizika jana nchini Zambia. Kambi hiyo ya siku tatu na nusu imewezeshwa na  Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) la nchini Israel. *****************************************************************************************************************************************************...

Watu 573 wafikiwa na huduma ya tiba mkoba Tabora

Image
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Buriani akizungumza na wataalamu wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati akipokea taarifa ya upimaji wa magonjwa ya moyo ujulikanao kama Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoa uliokuwa ukifanyika mkoani Tabora na kumalizika mwishoni mwa wiki iliyopita.  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Dkt. Batilda Buriani akimkabidhi zawadi za wataalamu wa afya waliofanya kambi ya upimaji wa magonjwa ya moyo mkoani humo Daktari kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Parvina Kazahura baada ya kumalizika kwa kambi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita. Wapili kulia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Tabora – KITETE Dkt. Mark Waziri Na: JKCI ********************************************************************************************************* Watu 573 wamepatiwa huduma ya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo katika kambi maalumu ya matibabu ijulikanayo kwa jina la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services iliyofan...